Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Shirika la Hilali Nyekundu limetangaza kuwa hadi sasa hafla (Marasimu) ya kuaga Kiongozi Shahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, imeendelea bila kuripotiwa majeruhi yeyote, licha ya mamilioni ya waombolezaji kushiriki katika tukio hilo la kihistoria.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wananchi wote wameendelea kushiriki katika shughuli za maombolezo kwa utulivu huku wakizingatia maelekezo ya usalama na kujitunza, jambo lililochangia kufanikisha uendeshaji wa tukio hilo bila matatizo makubwa.
Shirika hilo limesema kuwa mafanikio hayo yametokana na maandalizi na usimamizi mzuri wa hafla hiyo pamoja na ushirikiano mkubwa wa waombolezaji na taasisi mbalimbali zinazohusika na huduma za dharura, na kulielezea tukio hilo kuwa moja ya matukio makubwa ya kihistoria yaliyosimamiwa kwa utaratibu na nidhamu ya Hali ya juu ya kiusalama.

Your Comment